Ulinganishaji wa Mofolojia ya Uambishaji wa Vitenzi Kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu

dc.creatorJuma, Mwanahija Ali
dc.date2021-12-20T09:12:59Z
dc.date2021-12-20T09:12:59Z
dc.date2019-12
dc.date.accessioned2023-11-03T09:34:17Z
dc.date.available2023-11-03T09:34:17Z
dc.descriptionTasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo.
dc.descriptionTasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo. Kimakunduchi ni lahaja inayozungumzwa kusini ya kisiwa cha Unguja kilichopo Zanzibar nchini Tanzania. Kitumbatu ni lahaja inayozungumzwa kaskazini ya kisiwa cha Unguja kilichopo Zanzibar Tanzania na Kiswahili sanifu ni lahaja iliyosanifiwa na kutumika katika maeneo yote rasmi popote duniani. Lahaja hizi tatu zina vitenzi vyenye viambishi kabla na baada ya mzizi wa kitenzi. Katika utafiti huu tumeshughulikia viambishi vya nafsi, viambishi vya njeo na viambishi vya yambwa. Kazi hii imetumia nadharia ya Umbo Upeo katika kubainisha mofolojia ya vitenzi, kufafanua mashartizuizi ya viambishi na kuyalinganisha katika Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Utafiti umebaini kuwapo kwa mlingano mkubwa wa mashartizuizi kati ya Kimakunduchi na Kitumbatu, pia mlingano kwa kiasi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu na tofauti chache kati ya lahaja hizo. Nadharia ya Umbo Upeo inashughulikia masuala ya kifonolojia ambayo yalionekana kujitokeza katika muundo wa sauti. Hata hivyo baadae nadharia hii imetumika katika kushughulikia masuala mengine ya kiisimu kama vile sintaksia, semantiki, mofolojia, isimujamii, isimu historia na taaluma nyingine kwa lengo la kuvibainisha vipengele vya kiisimu vilivyomo katika matawi hayo ya kiisimu kwa kuzingatia misingi mitatu ambayo ni Uzalishaji, Mashartizuizi na Tathmiini. Vilevile, huangalia jinsi lugha inavyopokea na kuzalisha vipashio mbalimbali vikiwemo mofu na kuvibainisha mashartizuizi yake na mwisho kuvifanyia tathmini kwa kuangalia ukubalifu, uhafifu au kutokukubalika kwa vipengele hivyo katika lugha inayohusika
dc.descriptionTHE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR
dc.formatapplication/pdf
dc.identifierhttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/180
dc.identifier.urihttps://zarip.planningznz.go.tz/handle/123456789/87
dc.languageother
dc.publisherTHE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR
dc.titleUlinganishaji wa Mofolojia ya Uambishaji wa Vitenzi Kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu
dc.typeThesis

Files