Uchambuzi wa Nyimbo za Uganga wa Pepo Zanzibar:

No Thumbnail Available

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

The State University of Zanzibar (SUZA)

Abstract

Description

Available in print form, Tunguu Reference Library
Kazi hii inahusu Uchambuzi wa Nyimbo za Uganga wa Pepo Zanzibar: Mtindo na Dhima zake (mfanokutoka jamii ya Watumbatu). Katika tasnia hii nyimbo za uganga wa pepo wa aina tatu zilikusanywa na kuchambulia. Nyimbo hizi ni za uganga wa pepo wa maruhani, rubamba, na puuwo. Utafiti huu ilifanywa katika vijiji vya Chaani Masingini, Mkwajuni, Kibeni na Tumbatu Kichagani. Katika maeneo hayo uganga ulihusika unafanywa sana na wakaazi wake. Lengo kuu la utafifi huu lilikua ni kufanya uchambuzi wa mtindo na dhima wa nyimbo za uganga wa pepo. Waganga, wari na wataalamu wa fasihi ya Kiswahili walitumiwa kutoa taarifa juu ya uganga na nyimbo zake. Watoa taarifa hawa walikua wazee na vijna – Wanawake na wanaume. Katika uchambuzi, tulichambua vipengele vya mtindo wa nyimbo za uganga wa pepo kwa kutumia njia ya maelezo. Tulitumia mbinu ya umakinifu (ushuhudiaji) na mahusiano au usaili katika kukusanya data za utafiti. Aidha katika uchambuzi wa nyimbo za uganga wa pepo tulitumia nadharia za muundo, dhima na kazi. Nadaria hizi zilifanikisha sana katika kusaidia uchambuzi wa nyimbo hizo. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa nyimbo za uganga wa pepo zimetungwa na kuimbwa kwa kutumia vipengele vya matumizi ya maneno, takriri neno, anaphora, epifora, tasai, taksila, tasako, tempo na sauti, usamamba, tanakuzi, mtindo wa nyimbo huru, mtindo wa kutumia mshororo mmoja, na mtindo wa kupokezana katika uimbaji. Kila mtindo ulikua na dhima zake kama vile kusisitiza jambo, kuvutia hadhira, kudokeza asili ya wimbo na kufanya wimbo kuimbika na kuhifadhika kwa uhalisia. Aidha tulibaini kuwa nyimbo hizi zilikua na dhima mbali mbali kama vile kubembeleza, kujuvya, kuchombeza na kuhamasisha.

Keywords

1.

Citation