Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa:

dc.creatorMOHAMED, Omar Salum
dc.date2020-08-18T08:00:07Z
dc.date2020-08-18T08:00:07Z
dc.date2018-01
dc.date.accessioned2023-11-03T09:33:56Z
dc.date.available2023-11-03T09:33:56Z
dc.descriptionAvailable in print form, Tunguu Reference Library
dc.descriptionUtafiti huu unahusu ‘Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa’. Mashairi ya nyimbo kadhaa wa kadhaa za taarab yamechunguzwa. Uchunguzi ulianzia na mashairi ya nyimbo za taarab halisi ambayo yametumika kama kigezo msingi katika kutambulisha usasa wa mashairi ya taarab ya sasa. Utafiti umefanyika katika wilaya tatu za Tanzania Visiwani na wilaya mbili za Tanzania Bara. Kwa upande wa visiwani ni Wilaya ya Chake Chake iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na Wilaya ya Mjini katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kwa Bara, ni Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Kinondoni, Daressalaam. Malengo ya utafiti huu yalikuwa matano. La kwanza, kuainisha sifa bainifu za mashairi ya taarab halisi. La pili ni kudhihirisha mambo yaliyobadilika katika mashairi ya taarab ya sasa. La tatu ni kupambanua sababu za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La nne, kutathmini athari za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La tano ni kuchunguza namna wasanii na wapenzi wa nyimbo za taarab wanavyoyapokea mabadiliko ya fani na maudhui yaliyomo kwenye mashairi ya taarab ya sasa. Data ilipatikana kupitia mbinu ya ushiriki nafsia, mbinu ya mahojiano, mbinu ya dodoso na mbinu ya kuwa na mtafiti msaidizi. Pamoja na mbinu hizo utafiti ulitumia Nadharia ya Uamilifu, Nadharia ya Semiotiki na Unadharia Unaozama, pamoja na Mkabala wa Utafsiriji wa Vitendo na Mkabala wa Kiislamu. Watafitiwa walikuwa watunzi wa mashairi, waimbaji, wapiga ala za muziki pamoja na washabiki/wapenzi wa muziki wa taarab. Uchambuzi wa data umeonesha kuwa ni kweli kabisa kwamba pana usasa wa waziwazi kwenye mashairi katika taarab ya sasa. Usasa huo ndio msingi uliyoshusha hadhi ya mashairi ya taarab ya sasa na kuwa maneno tu. Vile vile, muziki huo utambulikanao kama taarab ya sasa wakosa vigezo thabiti vyenye kuyakinisha uhalali wa kuitwa taarab.
dc.formatapplication/pdf
dc.identifierhttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/148
dc.identifier.urihttps://zarip.planningznz.go.tz/handle/123456789/36
dc.languageother
dc.publisherThe State University of Zanzibar (SUZA)
dc.subject1. Sifa bainifu za mashairi ya taarab halisi 2. Mabadiliko katika mashairi ya taarab ya sasa - Sababu na athari
dc.titleUsasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa:
dc.titleFani na Maudhui
dc.typeThesis

Files