Ushikamano wa Sentesi katika Riwaya za Kiswahili: Ulinganishi wa Nyota Rehema na Utengano

No Thumbnail Available

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

The State University of Zanzibar (SUZA)

Abstract

Description

Available in print form, Tunguu Reference Library
Ushikamano ni dhana ya kisemantiki, ambayo hurejelea tabia au sifa za vipashio vikubwa zaidi ya mofimu, vinavyoambatanishwa pamoja katika sentensi ili kuunda matini. Dhana hii kwa muda mrefu imeonekana kama kuwa haiwezi kuangaliwa katika matini za fasihi, badala yake huangaliwa katika matini nyengine tu ambazo si za fasihi. Lengo la utafiti huu ni kuchunguza ushikamano wa kisarufi katika riwaya za Kiswahili, ikitolewa mifano kutoka katika riwaya za Nyota ya Rehema iliyoandikwa na Mohamed Suleiman Mohamed, mwaka 1976; na Utengano, iliyoandikwa na Said Ahmed Mohammed mwaka 1980. Data za utafiti huu zimepatikana kwa njia ya kudurusu riwaya hizo, na makala mbalimbali zilizosaidia kupatikana kwa data sahihi. Utafiti huu umebaini kuwa waandishi wa riwaya za Nyota ya Rehema na Utengano wametumia vijenzi vya ushikamano vya aina nne katika kazi zao. Vijenzi hivyo ni urejeleaji, udondoshaji, ubadilishaji na uunganishaji. Utafiti huu utasaidia kutoa mwangaza kwa watafiti kuchambua kazi za fasihi kwa kutumia vipengele mbalimbali vya kiisimu. Vilevile utasaidia kuwakumbusha waandishi kuwa isimu na fasihi ni taaluma zenye uhusiano wa karibu hivyo katika uandishi wao waangalie taaluma zote mbili wasiegemee upande mmoja.

Keywords

1. Ushikamano wa kisarufi katika riwaya za Kiswahili - Nyota ya Rehema, Utengano

Citation