Matumizi ya Lugha ya Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili

No Thumbnail Available

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

SUZA

Abstract

Description

Utafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili.
Utafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika kukusanya data za maktabani, mtafiti alifanya uchunguzi na uchambuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia makala mbalimbali zinazohusiana na utafit huu. Kwa upande wa data za uwandani, mtafiti alitumia mbinu ya usaili, hojaji na uchunguzi makinifu kwa kutumia usampulishaji mdokezo na lengwa. Katika kuzichambua data hizo, mtafiti alitumia mkabala wa kiidadi na mkabala stahilifu. Hata hivyo, mikabala yote ilitumika pale palipohitajika. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ilitumika kuchambulia data zinazohusiana malengo mahsusi ya utafiti huu na Nadharia ya Maana ni Matumizi ilitumika kuchambua data kwa pale panapostahiki. Matokeo ya utafiti huu, yaliweza kutupatia sifa tafauti za kiuzungumzaji katika maneno na mitindo ya sentensi katika kipengele cha sauti, maneno, sentensi na maana. Pia utokeaji wa lugha ya Kiswahili katika miktadha mbalimbali unatafautiana kimaana na kimuundo na unafafana katika utumiaji wa baadhi maneno na kwa upande wa kiisimu tuliweza kubaini changamoto hasi katika fonolojia, mofolojia, sintaksia na msamiati na chanya katika semantiki na msamiati, aidha kwa upande usio wa kiisimu tuliweza kupata changamoto hasi zaidi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mtafiti anapendekeza kuwa jamii itoe taaluma maalumu itakayoshughulikia kuthibiti na kuhifadhi matumizi sahihi ya lugha.
SUZA

Keywords

1. Matumizi ya Lugha ya Vijana - Kiswahili 2. Lugha - Kiswahili 3. Changamoto za lugha - Vijana wa Kizanzibar

Citation