Aina za Usambamba na Dhima zake katika Riwaya Teule za Kiswahili
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Utafiti huu wenye anuani: Aina za Usambamba na Dhima zake katika Riwaya Teule za Kiswahili umeangalia dhima za usambamba katika riwaya nne teule za Kiswahili; Nyota ya Rehema (1975), Kiu (1972), Ukiwa (1976) na Mafuta (1985). Mbinu ya usambamba ni moja wapo ya kipengele muhimu sana katika kazi mbalimbali za fasihi. Mbinu hii hutumiwa zaidi katika fasihi yenye mwelekeo wa kishairi kama vile mashairi na tenzi. Katika nathari mbinu hii imekuwa pia ikitumika lakini bila kupewa umuhimu unaostahiki kutoka kwa waandishi na wachamabuzi. Sio wachambuzi wengi walioshughulikia mbinu hii katika tahakiki zao. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza aina na dhima za usambamba katika riwaya teule za Kiswahili. Aidha mazingira ya kutokea kwa mbinu ya usambamba katika riwaya hizo pia yalichunguzwa. Data za msingi za utafiti huu zilikusanywa kutokana na udurusi wa riwaya teule na data za sekondari zilikuwa ni maoni ya wasailiwa zilizokusanywa kwa njia ya usaili, hojaji na majadiliano kimakundi.Utafiti uliongozwa na nadharia mbili; nadharia ya umuundo iliyotumika kuangalia usambamba na aina zake na nadharia ya uamilifu ambayo imetumika kuangalia dhima za usambamba katika riwaya zilizochunguzwa. Uchunguzi umebaini kuwepo kwa aina mbalimbali za usambamba wenye dhima anuai. Aina hizo zilibainika kujitokeza katika mazingira maalumu katika matini.. Utafiti huu umekuwa na umuhimu mkubwa katika fasihi ya Kiswahili hasa kwa kuwa umetumia misingi ya kilughawiya kuichambua fasihi ya Kiswahili. Aidha pamepatikana utafiti umeibua mwamko juu ya kuvishughulikia vipengele vya kifasihi vilivyopuuzwa kwa muda mrefu. Baada ya utafiti huu, ipo haja ya kufanyika kwa tafiti nyingine za kiusambamba katika tanzu nyingine za fasihi andishi kama vile tamthilia na hadithi fupi.

Keywords
1. Dhima za riwaya teule - Nyota ya Rehema, Kiu, Ukiwa na mafuta 2. Usambamba wa riwaya teule - Nyota ya Rehema, Kiu, Ukiwa na mafuta