Ripoti Kuhusu Utozaji Kodi Shughuli ya Uvuvi wa Bahari Kuu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2018-08-11
Authors
Tanzania Revenue Authority ( TRA )
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Tanzania Revenue Authority(TRA)
Abstract
Kumekuwa na haja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na wadau wengine wanaofuatilia makusanyo ya Serikali pia na Waheshimiwa Wabunge kuona kuwa shughuli za uvuvi katika Bahari Kuu zinaongeza mchango wake katika mapato ya Serikali hasa mapato yatokanayo na kodi. Msukumo huo umepelekea uwepo wa juhudi mbalimbali tangu mwaka 2003 ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Taasisi nyingine za Serikali kama Ofisi ya Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Wizara ya Kilimo na Uvuvi kutaka kupata mapato ya kodi yatokanayo na Uvuvi wa Bahari Kuu. Juhudi hizi zimehusisha kufanya tafiti mbali mbali, kufanya vikao na wadau wa Sekta hii pamoja na kufanya ziara ya kupata uzoefu kutoka nchi zingine zenye Uvuvi wa Bahari Kuu zikiwemo Kenya, Msumbiji na Ushelisheli kwa lengo la kuona ni namna gani nchi hizo zinavyopata mapato kutoka kwenye Sekta ya uvuvi wa Bahari Kuu. Kufuatia juhudi hizi, TRA ilitoa mapendekezo kadha wa kadha yanayolenga kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na rasilimali samaki walioko katika Ukanda Maalumu wa Uchumi (EEZ) wa Tanzania ili kuchangia katika pato la Taifa. Mbali na juhudi hizo za pamoja, TRA imekuwa na juhudi zake za ndani za kutaka kujua namna bora ya kupata mapato ya Serikali kutokakwenye uvuvi wa Bahari Kuu.
Description
Keywords
Citation
Collections